Overblog
Edit post Follow this blog Administration + Create my blog
PK ONLINE NEWS

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwandosya, ampa Wasira

September 10 2018 , Written by pascal kadushi

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwandosya, ampa Wasira

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Stephen Masato Wasira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
Wasira anachukua nafasi ya Prof. Mark James Mwandosya.
Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Festus Bulugu Limbu kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (National Economic Empowerment Council – NEEC).
Dkt. Limbu anachukua nafasi ya Dkt. John Jingu ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto).
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 9 Septemba, 2018

Share this post
Repost0
To be informed of the latest articles, subscribe:
Comment on this post